Wanawake wa kenya kufanya maandamano

Image caption Mwanamke aliyevuliwa nguo na makondakta katika kituo kimoja cha kuegesha magari nchini kenya kwa kudaiwa kuvaa nusu uchi.

Kundi la akina mama wa kilimani waliopo katika mtandao wa facebook nchini Kenya limeapa kufanya maandamano katika bustani ya Uhuru Park tarehe 17 mwezi huu ili kuungana na mwanamke aliyevuliwa nguo hadharani siku ya jumatano kwa kuvaa nusu uchi mbali na kupinga unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake.

Katika kisa hicho kilichofanyika katika kituo cha kuegesha magari cha Embassava jijini nairobi,wanaume wanaodaiwa kuwa makondakta wa matatu walimvua nguo mwanamke huyo na kusema kwamba alikuwa anawasisimua kwa mavazi yake.

Wanawaake hao wameapa kuelekea katika kituo hicho cha magari ya uchukuzi ili kuwaambia makondakta hao kwamba wanawake wana haki ya kuvaa wanavyotaka.

Kanda ya video ya kisa hicho ilichukuliwa na baadhi ya wasafiri na kuwekwa katika mtandao wa jambo net.

Wakenya pia wamepinga tukio hilo kupitia neno MyDressMyChoice katika mtandao wa twitter.

Wanaume wengi wamesema kuwa watajiunga na wake zao pamoja na wana wao wa kike kupinga uhalifu huo siku ya jumatatu.