Utata kuhusu kuuawa kiongozi wa IS

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi wa IS Abu Bakr Baghdadi anayedaiwa kuawa na sauti yake iliyorekodiwa kusikika tena

Dola ya Kiislam Islamic State imesambaza sauti iliyorekodiwa wanayodai ya Kiongozi wao.

Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Marekani dhidi ya wapiganaji wa dola ya Kiislam ambapo ilidaiwa yalimuua au kumjeruhi vibaya kiongozi wao Abu Bakr Al Baghdadi .

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Marekani amesema hawezi kuthibitisha ukweli wa sauti hiyo ambayo imeweka kumbukumbu na matukio yaliyotokea tangu siku ya kwanza ya mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya dola ya kiislam.

Kumbukumbu hizo ni pamoja na Tangazo la Rais Barack Obama la kuongeza wanajeshi zaidi nchini Iraq na ahadi mpya kwa wapiganaji kuwaunga mkono wapiganaji kutoka Libya, Yemen, na Misri