Wazazi waendeleza maandamano Mexico

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji Mexico

Wazazi wa wanafunzi 43 wa Mexico waliotoweka wiki 7 zilizopita wameendelea kuandamana dhidi ya serikali.

Wazazi hao walifunga msafara wa basi litakalowazungusha nchi nzima wakielezea kutoridhika kwao na jinsi serikali inavyolishughulikia suala hilo.

Waandamanaji wengine wamejiunga nao wakipeperusha mabango na picha huku wakiupungia mkono msafara huo ulioanzia jimbo la Guerrero.

Wiki iliyopita maafisa wa Mexican walithibitisha kwamba Genge la wahalifu walikiri kuwa waliwauwa wanafunzi hao na kuchoma miili yao, cha kushangaza ni kuwa awali wanafunzi hao walikuwa wamekamatwa na kuzuiliwa na polisi baada ya kufanya mgomo huko mjini Iguala.

Hadi sasa miili yao haijapatikana.