Miili ya raia wa A Kusini yarejeshwa

Jumba la kanisa lilopromoka Lagos Haki miliki ya picha AP

Miili ya raia 74 wa Afrika Kusini ambao walikufa wakati nyumba ya kanisa ya kupokea wageni ilipoporomoka nchini Nigeria, imerejeshwa nyumbani miezi miwili baada ya kufariki.

Ndege ya kubeba mizigo ilipeleka miili hiyo kwenye kituo cha jeshi la wanahewa nje ya Pretoria.

Serikali ya Afrika Kusini ilisema miili ilichelewa kurejeshwa kwa sababu ilichukua muda kutambua mabaki ya miili ya watu hao ambayo ilivurugika chini ya kifusi.

TB Joshua, kiongozi wa kanisa Synagogue Church of All Nations, ambalo likimiliki hiyo nyumba iliyoporomoka mjini Lagos, alieleza watu waliokufa kuwa mashujaa wa ufalme wa Mungu.

Serikali ya Afrika Kusini inasema jumla ya watu waliokufa ni 116.