Achumbia mwanamke akidhani ni mwanamume

Haki miliki ya picha Ankit Srivastva
Image caption Watu waliobadili jinsia huko Allanabad

Msichana aliyempenda mpenziwe wa dhati nchini Uingereza hakuamini alipogundua kuwa mwanamume huyo alikuwa amezaliwa msichana.

Mwanamke huyo hakugundua licha ya kuwa na uhusiano na mwanamume kwa jina Kieran Moloney ambaye alizaliwa na kuitwa jina Ciara.

Maumbile ya kiume ya jamaa huyo yalimuhadaa binti huyo kwa siku nyingi sana.

Kwa miaka mingi Moloney alificha siri hiyo hadi alipokutana na mwana dada huyo Charlotte mwaka 2012.

Lakini licha ya kisa hicho cha kushtua wawili hao wameamua kufanya harusi huku wakitumia mbegu za kiume zilizotolewa na rafikiye Moloney.

Charlote amesema kuwa hakudhani kuwa mpenziwe alizaliwa mwanamke lakini alipomueleza aliona hakuna makosa.

Haki miliki ya picha EITAN ABRAMOVICHAFP
Image caption Mtu aliyebadili jinsia yake.

Alisema kwamba anampenda vile alivyo kama mwanamume.

Aliongezea ,'' ana maumbile ya kiume na mwili mzuri na pia ni rafiki yangu''.

''Sijakuwa na wasiwasi kuhusu kuwa na mpenzi aliyebadilisha jinsia yake.''alisema Charlotte.

Lakini Moloney ambaye chimbuko lake ni nchini New zealand kwa sasa anasema kwamba alipukutana na Charlotte alivutiwa na urembo wake,lakini akawa na wasiwasi wa nini kingetokea iwapo angemgundua kuwa mwanamke.