Ajikata uume akitaka kuwa mwanamke

Image caption Wengi wamehoji kwanini mwanamume huyu amejikata uume wake badala ya kwenda hospitali kwa upasuaji

Msanii Mrusi aliyecheza katika filamu mashuhuri ya 'Burnt by the Sun 2', alipoteza uume wake baada ya kujikata akitaka kuwa mwanamke.

Kikubwa kilichomfanya msanii huyo Evgniv Sapaev kujitaka sehemu zake za siri ni kwamba alitaka sana kuwa mwanamke.

Mwanamume huyo alionekana akotoka nje ya nyiumba yake huku damu ikimwagika kutoka kwa sehemu zak nyeti kufuatia upasuaji aliojifanyia mwenyewe.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye nyota yake ilikuwa inang'ara sana alikimbizwa hospitalini kwa huduma ya dharura kwa hofu ya hali yake kuwa mbaya .

Madaktari walijaribu kumshona lakini hawakufanikiwa katika juhudi zao za kumrejeshea mwanamume huyo uume wake.

Afisaa mmoja hospitalini ambako muigizaji huyo alipokea matibabu alisema alikuwa na bahati sana kuponea kwani alivuja damu nyingi na kwamba angepoteza muda kidogo tu angefariki.

Kwa mujibu wa jarida la Mirror, jirani ya Evgniv Sapaev, Arkhip Tikhonov mwenye umri wa miaka 57 alishtuka sana alipombishia mlango na kujionea hali yake akiwa tayari ameanza kudhoofika kwani alikuwa amepoteza damu nyingi sana.

''Alionekana akitisha sana akiwa na damu mikononi mwake huku akishika sehemu yake ya uuma ambayo alikuwa ameikata. Nilidhani alikuwa anafanya mazoezi ya uigizaji, lakini alipozirai mlangoni huku akiwa ameshika sehemu yake ya siri mkooni ndipo nilipogudnua kuwa mambo yalikuwa mbaya,'' alisema jirani wa Evgniv

Baada yua kupata nafuu mwathiriwa alinukuliwa akisema, ''tangu niwe mtoto mdogo nimekuwa nikijihisi kuwa mwanamke. Nilijaribu mara nne kukata nyeti zangu lakini wakati wote sikuwa na ujasiri wa kufanya hivyo.Lakini wakati huu niliweza kufanya hivyo baada ya kumeza tembe za kuzuia maumivu, na kujitaka kwa kutumia kisu.

Badhi walimkosoa msanii huyo kuwa kujikata sehemu zake za isiri badala ya kwenda hospitalini kwa upasuaji.