China na Australia kushirikiana kibiashara

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa China Xi Jinping na waziri mkuu wa Australia Tony Abbot

Rais wa China, Xi Jinping ametia saini mpango wa biashara huru na waziri mkuu wa Australia Tony Abbott.

Makubaliano hayo yanayojiri baada ya majadiliano ya miongo kadhaa yatafungua masoko taratibu yenye thamani ya mabilioni ya dola.

Yatawanufaisha wakulima wa Australua na sekta za huduma na kupunguza vikwazo katika uekezaji wa China katika nchi hiyo yenye rasilmali tajiri.

Rais Xi aliliambia bunge la Australia kuwa lengo lake ni kuzidisha maradufu mapato ya taifa la Uchina ifikapo mwaka 2020 na kujenga nchi ya kisasa ya ujamaa.

Yeye ni kiongozi wa pili wa pekee kutoka Uchina kuwahi kuwahutubia wabunge Canberra.

Aliongezea kuwa Beijing imejitolea kuhakikisha kuwa amani imedumishwa,na wabunge walisimama kumpa heshma alipomaliza kusoma hotuba yake.

Makubaliano mapya ya kuanzisha soko huru yanatarajiwa kufungua masoko kwa wakulima wa Australia wanaouza nje ya nchi pamoja na sekta ya huduma na wakati huohuo kurahisisha vizuizi kwa uwekezaji wa Uchina katika nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali ya Australia.

Nje ya bunge,waandamanaji walitoa mwito kwa Rais Xi kupunguza udhibiti wa Uchina eneo la Tibet na kumaliza mateso dhidi ya makundi ya kidini.