Maaskofu wanawake kutawazwa Uingereza

Image caption Swala la kuidhinishwa maaskofu wa kike daima huzua mjadala

Kanisa la England linatarajiwa kupititsha rasmi sheria itakayo waruhusu maaskofu wa kike kuteuliwa kwanzia mwaka ujao.

Kikao cha viongozi wa dini kilipiga kura kurejesha mikakati wa kuwateua Maaskofu wa kike hapo mwezi wa saba.

Mapadri wa kwanza wa kike waliteuliwa 1994, lakini hadi sasa hawajaweza kupata majukumu makuu kanisani.

Mgawanyiko unazidi kuonekana katika kanisa la kianglikana kati ya wale wanaosema mchakato huo unaambatana na imani yao na wale wahafidhina wanaopinga.

Juhudu za hapo awali za kuwatawaza maaskofu wa kike zilishindwa kunawiri mwaka wa 2012, baada ya wanachama sita wa kawaida wa kikao cha viongozi, kikao kinachobuni sheria, kutounga mkono wazo hili la maaskofu wa kike.

'Utamaduni kubadilika'

Kura ya Jumatatu katika kakao cha viongozi huko church house Westminster itawezesha kupitishwa kwa muhuri wa mwisho wa sheria hiyo, itakayofuatwa na kupitishwa katika bunge mwezi Oktoba.

Mwandishi wa habari wa BBC wa maswala ya kidini Caroline Wyatt alisema kuwa "ni hatua ya kipekee katika huu mchakato wa muda mrefu lakini ni wazi kuwa ni mfano wa kihistoria sana na wa muhimu pia "

Maombi ya nafasi hiyo kutoka kwa wanawake tayari imepokelewa katika dayosisi za Nottingham na South well, ingawa hakutakuwa na habari zozote hadi Januari 2015

Gloucester, Oxford na Newcastle pia ni madayosisi ambayo maaskofu wapya wanatarajiwa kuteuliwa.

Uamuzi huu umepokelewa vyema na wale waliokuwa wakikampeni kwa muda mrefu, inaonekana kuwa ni njia nzuri ya kuongeza ushiriki wa wanawake kanisani.

Mchungaji mkuu Jane Hedges wa Norwich amesema kuwa hapo awali alidhani kuwa mchakato huu hautafanyika hadi kustaafu kwake.

Alifikiria kuwa "watu walishangazwa jinsi wanawake wamekubalika kwa haraka kwa kama mapadri" aliongezea kuwa njia ya kukuwa padri ingechukua muda mrefu.

Kwa sasa wanawake wanakarabia 35% katika uongozi wa kanisa.

'Sio muafaka'

Katika mwezi wa Oktoba, kanisa lilisema kuwa ubaguzi chanya unaweza kutumika kuwaweka maskofu wa kike ambao hawajawakilishwa vizuri.

Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby amepongeza kura ya kihistoria iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu kama "ni mwanzo wa tukio kubwa linaloweza kushamiri ama linalotatanisha"

lakini hatua hii ya kuteuwa maaskofu wa kike haitapokelewa vyema duniani.

Kitengo kinachopinga mchakato huo - the conservative evangelical group Reform - wanasisitiza kuwa "amri ya uongozi wa kiume katika kanisa inakataza wanawake kuwa viongozi katika madayosisi"

Mageuzi haya yanakadiria kuwa robo ya makanisa itapata kuwa hayambatani na imani zao.

Sheria hii inajumuisha miundo ya kusimamia watu wenye maoni tofauti kwa mfano kubuni wakaguzi huru watakaosimamia mipangilio ya parokia zinazohitaji uangalizi wa Maaskofu wa kiume.