Netanyahu aishutumu Palestina na Hamas

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amewataka Waisrael kuungana bila kujichukulia sheria mkononi baada ya Wapalestina wawili wakiwa na bunduki na mashoka kuwaua waumini wanne katika hekalu moja mjini Jerusalem.

Ameyashutumu Mamlaka ya Palestina na Hamas kwa kuchochea shambulio hilo. Lakini maafisa wa Palestina wamemlaumu Netanyahu kwa kuchochea ghasia kubwa za hivi karibuni, zilizosababisha Waisrael na Wapalestina kuuawa.

Amesema kama taifa watakabiliana na ugaidi na wafadhili wao.Hata hivyo Netanyahu ameongeza kuwa kwa sasa wapo katika kampeni ndefu ya vita dhidi ya ugaidi na ambayo haikuanza leo.

Netanyahu amesisitiza kuwa kuna watu baadhi ya watu wanaotaka kuwandoa katika mji mkuu wa Israel Jerusalem, suala ambalo amesema haliwezekani kwani huo ni mji mkuu wao milele.