BBC kutangaza fainali za Langa langa

Image caption Langa Langa

Kilele cha mashindano magari ya langa langa ya Formula 1 kwa msimu wa mwaka 2014 yatakayofanyika Abu Dhabi yanaweza kufuatiliwa moja kwa moja katika matangazo ya BBC ya televisheni, radio na mtandao wa internet.

Hatua ya mwisho ya kampeni ya mbio za 19 katika uwanja wa Yas Marina utaamua hatima ya taji linalowaniwa na madereva wawili baada ya kuchuana kwa miezi tisa kati ya madereva wa timu moja ya Mercedes ambao ni Lewis Hamilton na Nico Rosberg.

Hamilton anaongoza kwa pointi 17 mbele ya Rosberg wakielekea katika hatua ya mwisho ya kuamua nani bingwa tarehe 23 Novemba, lakini kutokana na utata wa pointi mbili katika mchezo kuna uhakika wa kubadilika msimamo kabla ya bendera ya mwisho kuinuliwa.

Mashindano ya Abu Dhabi Grand Prix yatatangazwa moja kwa moja katika televisheni ya BBC, wakati ambapo kutakuwa na kutangazwa katika radio na mtandaoni, ikiwa ni pamoja na sauti za radio na uchambuzi.

Unaweza kupata matokeo ya mbio hizo za magari ya langa langa kutoka BBC Sport app, ikiwa na maana kwamba unapata matokeo kadiri yanavyotokea.

ABU DHABI GRAND PRIX - WAKATI WA KUANGALIA

Ijumaa 21 Novemba

02:55-10:35, Asubuhi BBC Two na BBC Radio 5 live sports extra, Practice 1.

7:00-8:35, Mchana BBC Two na BBC Radio 5 live sports extra, Practice 2 na kuendelea katika siku za Jumamosi Novemba 22 na Jumapili Novemba 23.

Kwa taarifa zaidi kuhusu mashindano haya, fuatilia matangazo yetu katika televisheni, radio na internet.