Gavana atangaza hali ya hatari, Missouri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Machafuko Missouri

Gavana wa jimbo la Missouri nchini Marekani ametangaza hali ya hatari kabla ya kutolewa uamuzi muhimu kuhusu kumfungulia mashitaka ya jinai au la dhidi ya afisa wa polisi mzungu, ambaye alimuua kwa kumpiga risasi kijana wa Kiafrika ambaye hakuwa na silaha.

Mauaji hayo yaliyotokea katika mji wa Ferguson mwezi Agosti yalisababisha vurugu katika mitaa kwa siku kadha na kuamsha mjadala kuhusu uhusiano kati ya polisi na jamii ya watu weusi nchini Marekani.

Idara ya polisi ya Kaunti ya St. Louis ndiyo wanaosimamia maandamano yoyote. Meya wa St. Louis, Francis. Slay, amezungumzia kuhusu tahadhari wanayochukua.