Urusi imelalamikia nchi za Magharibi

Image caption Dmitry Peskov Msemaji mkuu wa Rais nchini Urusi

Msemaji mkuu wa Rais wa Urusi Dmitry Peskov amezituhumu nchi za magharibi kwa kujaribu kuizunguka nchi hiyo.

Katika mahojiano na BBC Peskov AMESEMA Urusi itapenda kusikia asilimia 100 ya ahadi kuihusiana na mzozo wa Ukraine.amesisitiza kuwa hakuna mtu aliyefikiria kuwa Ukraine ungejiunga na NATO. Amesema hili liliwapa hofu na kuifanya Urusi kuwa na tahadhali kubwa wakati kuhusiana na mgogoro wa Ukraine. Awali waziri wa kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier alionya kuwa Ulaya wanakabiliwa na upinzani zaidi kuliko kuleta umoja. Steinmeie ametoa maoni yake kufuatia mazungumzo kati yake na Waziri mwenzake wa kigeni Sergei Lavrov wa Ujerumani.