Ndoa ya mpiganaji wa IS yavunjika

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mama wa Aicha

Mama raia wa Uholanzi amefanikiwa kurejea na binti yake aliyekuwa ameolewa na mpiganaji wa kundi la Kiislam la IS na kuishi katika mji wa Raqqa ambao ni ngome kubwa ya wapiganaji hao wa Islamic State.

Msichana huyo Aicha aliondoka Uholanzi Februari mwaka huu na kwenda Syria kuolewa na mpiganaji wa kundi hilo mwenye mchanganyiko wa uraia wa Mholanzi na Mturuki ambaye pia amewahi kufanya kazi katika jeshi la Serikali ya Uholanzi.

Haki miliki ya picha
Image caption Wapiganaji wa Islamic State

Hata hivyo ndoa hii haikudumu baada ya Aicha kutorishwa na mwenendo mzima wa maisha yao ya ndoa.

kutokana na utata wa ndoa hiyo ya binti huyo,mama yake mzazi ameamua kusafiri umbali mrefu na kwa gharama kubwa kumfuata bint yake ambaye wa binti huyo na kisha kurudi nae nyumbani.