Compaore aenda uhamishoni Morocco

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Blaise Coompamy

Nchi ya Ivory Coast imesema Rais wa Burkina Faso aliyeondolewa madarakani Blaise Compaore ameondoka nchini humo kwenda uhamishoni Morocco.

Compaore alikimbilia Ivory Coast mwishoni mwa mwezi uliopita kutokana na maandamano yaliyokuwa yakimtaka kuachioa madaraka.

Hata hivyo sababu nyingine iliyochangia kuondolewa madarakani kwa rais ya raia wa nchi Compaore ni pamoja na jaribio la kutaka kujiongezea muda wa utala wake

Haijafahamaika mara moja kama Compaore na familia yake wanatarajia kuishi maisha yao yote nchjini Morocco.