Maandamano makubwa kufanyika Mexico

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji nchini Mexico wakiwa na picha za wanafunzi 43 waliopotea kwa kutekwa katika jimbo la Guerrero

Wananchi wa Mexico wamekuwa wakikusanyika kabla ya maandamano makubwa yaliyopangwa kufanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Mexico City na miji mingine ili kupinga utekaji nyara wa wanafunzi arobaini na watatu.

Mikusanyiko mitatu ya maandamano itaungana katika lango la bustani kuu mjini Mexico City.

Waandamanaji wanaongozwa na ndugu wa wanafunzi waliopotea. Serikali inasema walitekwa nyara na polisi wanaohusishwa na genge la wauza mihadarati katika jimbo la kusini mwa Mexico la Guerrero. Huenda wanafunzi hawa waliuawa.Shughuli za biashara na maduka katika eneo hilo yamefungwa kama njia ya kuchukua tahadhari. Rais wa Mexico amesema nchi imeumizwa, lakini amani na haki ni mambo yanayotakiwa kusonga mbele