Obama kutangaza mabadiliko ya uhamiaji

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Barack Obama

Ikulu ya Marekani imesema Rais Obama atatumia muda ambao watazamaji wa televisheni nchini humo wanaangalia zaidi matangazo siku ya Alhamisi kutangaza mabadiliko makubwa ya mfumo wa uhamiaji wa nchi hiyo.

Inatarajiwa kuwa Rais Obama atasema kuwa atatumia madaraka yake aliyopewa kikatiba kuzuia wahamiaji wapatao milioni tano kurejeshwa makwao na badala yake wapatiwe vibali vya kufanya kazi nchini humo.

Rais Obama amesema hayo katika video iliyotumwa katika ukurasa wa facebook kabla ya hotuba yake.Tangu kuingia madaraka Obama amekuwa akipigania baadhi ya mabadiliko ikiwemo huduma ya utoaji wa huduma za afya kwa mfumo wa bima ya afya.