Polisi mashakani kwa kumpuuza mwathiriwa

Image caption Watu wengi nchini Afrika Kusini wanapoteza imani na polisi nchini humo

Polisi watatu nchini Afrika Kusini, wameachishwa kazi kwa muda kwa tuhuma za kukataa kumuokoa mshukiwa wa wizi aliyekuwa anashambuliwa na umma.

Mshukiwa huyo alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata.

Tukio hilo, lililonaswa kwa video, linaonyesha baadhi ya wakazi wa mtaa wa Delft mjini Cape Town wakimshambulia mwanamume huyo.

Maafisa wawili wa polisi waliokua wakila Ndizi walionekana wakitembea kando ya mwathiriwa bila kumsadia.

Huku kukiwa na visa vingi vya ufisadi, wengi nchini Afrika Kusini wanapoteza imani kwa polisi kuweza kuwatekelezea haki.

Maafisa katika mtaa huo wanasema kuwa kwa polisi kukosa kuchukua hatua itasababisha wakazi wa eneo hilo kukosa imani na polisi.