Wanaotumia dawa michezoni wafungiwe

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Varier Adams

Bingwa wa dunia Olimpik riadha Valerie Adams amependekeza kufungiwa maisha kwa mwanariadha atakayebainika kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.

"Udanganyifu ni udanganyifu tu hauna muamana" amesisitiza Adams, akiongeza kuwa hata kama itakuwa ni kosa la kwanza adhabu iwe hiyo hiyo.

Kwa sheria za sasa anayebainika kutumia dawa hizo michezoni anafungiwa kutoshiriki michezo kwa miaka miwili,adhabu ambayo inatarajiwa kuongezeka hadi miaka minne hapo mwakani.

Adams ni mmoja wa wanariadha wanawake aliyetajwa na shirikisho la riadha IAAF kuwania tuzo kwa mwaka huu.