Maandamano kupinga utekaji nyara Mexico

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wakipambana na vijana Mexico

Polisi wa kupambana na fujo mjini Mexico wamewazuia maelfu ya waandamanaji kutoka bustani ya mji mkuu huo wanaoandamana kupinga kutekwa nyara kwa wanafunzi 43.

Polisi wamechukua hatua hiyo baada ya kukabiliana na mamia kadhaa ya waandamanaji hao walijifunika nyuso zao nje ya ikulu.

Waandamanaji hao wanataka haki kwa wanafunzi wote 43 wanaongozwa na jamaa wa wanafunzi hao waliotekwa katika jimbo la kusini la Guerrero mnamo mwezi Septemba.

Serikali inasema polisi inayohusika na magengi ya madawa ya kulevya ndio waliohusika na huedna wanafunzi hao wameuawa.

Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto amesema nchi yake imeumizwa, lakini amani na haki ndio suluhu.

Awali polisi ililitawanya kundi la waandamanaji waliojaribu kuzuia barabara karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa mjini humo.

Walihesabu moja hadi arobaini na tatu kuwakilisha kila mwanafunzi na wametaka haki itendeke.