Wanawake wenye vyeo huzongwa na mawazo

Image caption Mwanamke aliyezongwa na mawazo.Utafiti unasema kuwa wanawake walio katika nyadhfa za juu kazini huzongwa na mawazo.

Wanawake huonyesha ishara za kuzongwa na mawazo kazini iwapo wanasimamia nyadhfa za juu ikilinganishwa na wanaume,kulingana na wanasayansi wa Marekani.

Miongoni mwa wanaume ,uwezo kama vile wa kuajiri na kupiga kalamu hupunguza ishara za kuwa na mawazo kulingana na Utafiti huo.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la afya na tabia za binaadamu uliwahoji wanawake na wanaume 2,800 walio katika umri wa kadri.

Mtafiti mmoja amesema kuwa utafiti huo unaonyesha umuhimu wa wanawake zaidi katika nyadhfa kuu.

Wanasayansi katika chuo kikuu cha Texas katika eneo la Austin waliwahoji wanaume 1300 na wanawake 1500 wa chuo kikuu cha Wisconsin katika simu mnamo mwaka 1993 na 2004 wakati walipokuwa katika umri kati ya miaka 54 na 64.

Watafiti waliwahoji walioshiriki kuhusu uwezo wao kazini mbali na siku katika juma lililopita ambapo walihisi kuzongwa na mawazo kama vile kuwa na hisia za kusikitisha na kufikiria kwamba maisha ya mtu yamefeli.

Lakini wakati kazi hiyo iliposhirikisha kupigwa kalamu kutumia ushawishi wake katika malipo,wanawake walionekana kupata ongezeko la mawazo kwa asilimia 9 ikilinganishwa na wanawake ambao hawako katika nyadhfa kuu.