Watu 28 wauawa kwa kupigwa risasi kenya

Image caption Wapiganaji wa kundi la Alshabaab wanashukiwa kuwaua takriban abiria 28 mjini Mandera nchini Kenya

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Alshabaab nchini Kenya wamewaua takriban watu 28 katika shambulizi la basi moja karibu na mpaka na Somali.

Waziri wa mswala ya ndani nchini Kenya amesema kuwa basi hilo lililokuwa na abiria sitini lilitekwa mjini Mandera lilipokuwa likitoka mjini Nairobi.

Inadaiwa kuwa abiria wasio waislamu walitengwa kutoka kwa abiria wengine na kupigwa risasi.

Ripoti nyingine zinaarifu kuwa mtu yeyote aliyeshindwa kusoma aya za Quran pia aliuawa.

Kenya imekumbwa na misururu ya mshambulizi ya risasi pamoja na mabomu yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la Alshabaab tangu vikosi vya Kenya kuingia nchini Somali mwaka 2011.