Al Shabaab lakiri kutekeleza shambulizi

Image caption Al Shabaab lakiri kutekelza shambulizi nchini kenya

Kundi la Al Shabaab nchini Somali linasema kuwa limefanya mashambulizi ya abiria 28 katika basi moja kazkazini mashariki mwa kenya.

Basi hilo ambalo lilikuwa likiwabeba abiria 60 lilitekwa katika jimbo la mandera lilipokuwa likelekea mjini Nairobi.

Abiria mmoja ambaye alinusurika ameiambia BBC vile raia wasio wa Somali walitengwa na wengine na wale ambao hawakuweza kusoma aya ya Quran walipigwa risasi kwa karibu.

Katika taarifa yake al Shabaab limesema kuwa mashambulizi hayo ni ya kulipiza kisasi mauaji ya waislamu huko Mombasa yaliotekelezwa na vikosi vya usalama vya kenya.

Kenya imekumbwa na misururu ya mashambulizi ya risasi na mabomu yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la Alshabaa tangu vikosi vyake viingie nchini Somali.