Ugaidi waingia michezoni

Haki miliki ya picha afp
Image caption Rais wa Afghanstan Ashraf Ghani

Mtu mmoja aliyekuwa amejifungasha kwa mabomu amejitoa muhanga kwa kushambualia mechi ya Volleyball mashariki mwa Afghanstan,na kuua watu wapatao arobaini na watano.

Msemaji wa Gavana wa jimbo la Paktika amesema watu wengine hamsini walijeruhiwa vibaya baada ya mtu huyo kujiripua katikati ya mashabiki wa mchezo huo.

Inasadikiwa kuwa watu wapatao miamoja walijitokeza kushuhudia mechi hiyo ya fainali ya kuwania kuingia katika michuano ya majji nchini humo.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililokubali kuhusika na shambulio hilo ingawa kuna shaka kwamba huenda kikundi cha kutoka nchini Taliban.

Naye raisi wa Afghanstan Ashraf Ghani ameelezea shambulio hilo kuwa si la kiutu wala si la kislam.