Raia wa Tunisia kumchagua rais mpya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia wapiga kura kumchagua rais wao mpya kufuatia kungatuliwa mamlakani kwa aliyekuwa rais Ben Ali

Wapiga kura nchini Tunisia wanaelekea katika vituo vya kupigia kura hii leo kumchagua rais mpya.

Huu ndio uchaguzi wa tatu kuandaliwa tangu mwaka 2011 wakati wa mapinduzi yaliyomuondoa madarakani rais Zine el-Abidine Ben Ali.

Mgombea mkuu kati ya wagombea wengine zaidi ya 20 ni Beji Essebsi wa chama cha Nidaa Tounes ambaye pia ni afisa wa zamani kwenye serikali ya rais wa Ben Ali.

Mpinzani wake mkuu ni rais wa sasa wa mpito Moncef Marzouki

Chama cha kiislamu cha Ennahda ambacho kilichukua nafasi ya pili kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba hakina mgombea.