Lewis Hamilton aibuka kidedea

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Lewis Hamilton na furaha ya ushindi, bendera ya nchi yake juu.

Dereva mwenye asili ya nchini Uingereza Lewis Hamilton ameshinda mbio za Abu Dhabi Grand Prix,na kumfanya dreva huyo wa mashindano ya Formula One kuwa mshindi wa mbio hizo kwa mara ya pili.

Hamilton alianza akiwa katika nafasi ya pili katika mashindano hayo, lakini baadaye akaanza kuongoza katika mbio hizo kutoka kwa mshiriki mwenziwe kutoka kampuni ya Mercedes, Nico Rosberg ili kutetea taji.

Hamilton mwenye umri wa miaka 29 ameshinda mara kumi na moja katika msimu huu.

Kwa mara ya kwanza Hamilton alishinda taji la mbio za Formula One mnamo mwaka 2008.

Hamilton alishinda mbio hizo baada ya gari aliyokuwa akiiendesha Nico Rosberg kupata tatizo katika engine.