Marufuku ya michezo kwa wanawake Iran

Haki miliki ya picha fivb.org
Image caption Hii ndo mechi ilomponza Ghonche Ghavami

Familia moja ya mwanamke mwenye asili ya Uingereza na Iran aitwaye Ghonche Ghavami,ambaye alitiwa korokoroni kwa kuthubutu kuangalia mechi ya mchezo wa Volleyball huko Tehran imeeleza kuwa mwanamke huyo yuko huru.

Ghavami alikamatwa mnamo mwezi June mwaka huu wakati wa maandamano nje ya uwanja wa Volleyball wakati ambapo timu ya taifa ya nchi hiyo ilipokuwa ikijiandaa kumenyana na Italy.

Mwanamke huyo alifungwa korokoroni kwa mwaka mmoja kwa kusambaza taarifa za kuipinga serikali ya nchi hiyo na kuandaa mgomo.

Inaelezwa kwamba wanawake wote nchini Iran wamepigwa marufuku ya kuhurudhuria matukio ya kimichezo ya wanaume.

Nayo bodi ya mchezo huo ya Iran ilinyimwa haki ya kuandaa michuano ya kimataifa ya mchezo huo kutokana na kukamatwa kwa mwanamk huyo.