Wanamgambo wawateka watoto 10 Mali

Haki miliki ya picha s
Image caption Mwanamgambo wa Mali

Maafisa wa kijeshi nchini Mali wanasema kuwa watu waliokuwa na silaha wamewateka nyara watoto kumi na kuwaua wawili ambao walijaribu kupinga kutekwa karibu na mji wa Kidal.

Afisa mmoja alisema kuwa watoto hao walilazimishwa kuwa wanajeshi.

Maeneo yanayozunguka mji wa Kidal yanadhibitiwa na kundi la kiislamu lililojitenga ambalo lilidhibiti eneo la kaskazini nchini Mali mwaka 2012 lakini baadaye likatimuliwa na wanajeshi wa Ufaransa kwa ushirikiano na vikosi vya muungano wa Afrika.