Polisi aondolewa mashtaka Marekani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waandamanaji wenye hasira wakilizonga gari la polisi

Ghasia zimezuka nchini Marekani, baada ya wanasheria kuamua kutomfungulia mashtaka polisi wa kizungu aliyeua kijana mweusi.

Vitu mbalimbali vinaarifiwa kuchomwa moto, baada ya jopo la Wanasheria nchini humo kuamua kutomfungulia mashtaka polisi huyo Daren Wilson, ambaye alimuua kwa kumpiga risasi kijana mweusi Michael Brown.

Tukio hilo lilitokea katika mji wa Ferguson mwezi Agusti mwaka huu.

Kwa upande wake Rais wa Marekani Barack Obama ametaka kuwepo kwa amani, licha ya kueleweka kwamba baadhi ya raia wa nchi hiyo watakuwa wamesikitishwa na kuingiwa na hasira na uamuzi huo wa Marekani.

Hapo awali kabla ya kutolewa kwa uamuzi huo, Gavana wa jimbo la Missouri Jay Nixon aliwataka watu kuwa wavumilivu na kupunguza jazba.