Andy Murray atangaza nia

Image caption mchumba wa Andy Murry ,Kim Sears.

Nyota wa mchezo wa Tennis Andy Murray amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa muda mrefu Kim Sears imeelezwa.

Murray, kwasasa ana umri wa miaka 27, na mpenziwe wamepishana mwaka mmoja Sears, 26, na mahaba yao yalianzaia mwaka 2005 na amekuwa shabiki wake mkubwa.

Inasemekana ombia la Andy nguli wa tenis katika viwanja vya Wimbledon alilitoa jana .

Lakini mapema mwaka huu Murray katika kipindi cha maswali na majibu baina yake na washabiki wake waliomuuliza endapo atakuwa tayari kumuoa mpenziwe mara baada tu ya fainali za Wimbledon.

Murry alitafakari kwa kina na baada ya saa moja aliwaambia mashabiki wake milioni mbili nukta tatu wanaomfutilia kwenye ukurasa wake wa twitter kwamba ana vitu vitatu vya kuwaambia mosi havuti majani, haowi hivi karibuni na hahitaji kumuua mpinzani wake Rafael Nadal.."

Lakini hatimaye amemtaka ruhusa mpenziwe Sears walodumu naye uchumbani kwa takriban miaka tisa ya kutaka kumuoa.

Sears, kwa taarifa tu ni binti wa aliyekuwa kiongozi wa shirikisho la tennis kwa upande wa wanawake Nigel Sears,na bibi Kim Sears alikutana na Murray katika mechi za ufunguzi za michuano ya US Open mnamo mwaka 2005.

Na nyota njema huonekana asubuhi, Kim anakubalika na mama yake Andy Judy Murray kusema endapo Murry atamuoa mwanamke huyo litakuwa jambo bora katika maisha ya mwanawe.