Maonyesho zaidi ya Cosby yaahirishwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanawake kadhaa wamejitokeza wakidai kudhalilishwa kijinsia

Maonyesho mawili zaidi ya muigizaji na mchekeshaji Bill Cosby yamefutwa wakati huu akishutumiwa kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Maonyesho yaliyopangwa kufanywa tarehe 29 mwezi huu katika jumba la maonyesho la Capital na tarehe 31 Mwezi Januari kwenye Ukumbi wa Foxwoods mjini Connecticut yameahirishwa

wanawake kadhaa wamejitokeza wiki za hizi karibuni wakimshutumu Cosby kuwadhalilisha kijinsia.

Muigizaji huyo hajazungumzia shutma hizo dhidi yake isipokua wanasheria wake ambao wamesema kuwa madai yao hayana ukweli na yanalenga kumchafua.

Kuahirishwa kwa maonesho hivi karibuni kumekuja baada ya kufutwa kwa onesho lililokuwa likitarajiwa kufanyika mjini Las Vegas wiki hii na maonesho mengine matano ya mwaka huu.

Mchekeshaji huyu anatarajiwa kuwa na maonyesho mawili tarehe 6 mwezi Desemba,katika kitongoji cha Tarrytown mjini New York pia atakuwa na maonesho mengine mwaka huu.