Chanjo ya Ebola yaonesha matumaini

Haki miliki ya picha NIAD
Image caption Chanjo ya Ebola katika majaribio,yafana

Wanasayansi wamepongeza matokeo ya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, na kusema dawa zinaonesha kuwa salama na itasaidia mfumo wa kinga ya mwili kuvitambua virusi hivyo.

Watu 20 waliojitolea kutoka nchini Marekani, walipatiwa kinga maradhi hiyo, ikiwa ni hatua muhimu ya kujikinga na virusi hivyo vya ugonjwa wa Ebola.

Utafiti wa chanjo hiyo ya ebola kama huenda ikaokoa maisha wa maelfu walio hatarini kuambukizwa virusi hivyo. Dr Anton Fauci ni mkuu wa Taasisi ya Marekani ya magonjwa ya kuambukiza :

"Kwa upande wa usalama na uwezo wa kuleta matokeo mazuri nadhani tunaweza kuita majaribio haya ya chanjo haikufanikiwa. Japokuwa katika mkondo wa awali imeonyesha mafanikio makubwa." Amesema Fauci

Hata hivyo watafiti wanasema matokeo hayo sio uthibisho kwamba chanjo hiyo inafanya kazi lakini kama majaribio ya awali yamekuwa na mafanikio basi chanjo ya eboal itatolewa kwa maelfu ya wafanyakazi wa afya huko Afrika Magharibi kuanzia mwezi Januari mwakani.

Zaidi ya watu elfu tano mia tano wamefariki kutokana na kuambukizwa virusi vya ebola.Kwa sasa chanjo imekuwa ikifanyiwa utafiti na kampuni GlaxoSmithKline.

Dr Colin Brown ni mtaalamu wa magonjwa ambaye amepokea habari za chanjo hiiyo kama habari njema.

"Kwa vile suala la usalama limepewa umuhimu tunayo furaha kwamba hakuna madhara yaliyotokana na chanjo. Ambapo imeonyesha wagonjwa wa awali wapatao 20 wakuwa na tatizo lolote. Ninadhani tutarajie kuona itasaidia hasa kwa upande wa wafanyakazi wa afya kujilinda wakiwa kazini. " Alisema Bwana Brown