Unaweza kuvaa nguo ya ndani ya mpenzi?

Image caption chupi

Je, unaweza kuvaa nguo ya ndani ya mpenzi wako?soma hii.

nguo ya ndani inayoweza kuvaliwa na watu wa jinsia zote sasa imeanza kuuzwa madukani nchini Marekani.

Hii ni baada ya kampuni moja nchini humo kuanza kutengeza nguo za ndani kwa lengo la kuhakikisha kuwa wapenzi wanaweza kutumia nguo moja bila tatizo lolote.

Kulingana na gazeti la the telegraph,nguo hizo kwa jina Play out zinazotengezwa na kampuni ya Abby Sugar na Sylvie Lardeux pia zinashirikisha suruali fupi zenye rangi ya kung'aa.

nguo hizo zimetengezwa kama za kiume lakini hazina zipu swala linalozifanya kuweza kuvaliwa na jinsia zote,ijapokuwa wengine wanaweza kulalama kwamba haziwapi faraja.

''Tunataka watu wajisike vizuri na wawe wenye raha wakati wanapovalia nguo hizi,lakini sio kuvaa ili kuwafurahisha watu wengine'', alisema bi Sugar ambaye amekuwa na uhusiano na Bi Lardeux kwa kipindi cha miaka mitano iliopita.

Wanasema kuwa waliamua kutengeza nguo hizo kwa kuwa wanaona mtindo wa chupi za wanaume kama zinazofurahisha na kuvutia .