Kijana mwingine mweusi auawa Marekani

Haki miliki ya picha ABC
Image caption Tamir Rice aliyeuawa

Polisi katika mji wa Cleveland nchini Marekani, wameachilia video inayoonesha mauaji ya kijana wa miaka kumi na miwili akipigwa risasi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kipande hicho cha video kinamwonesha Tamir Rice akipigwa risasi sekunde chache tu gari la polisi lilipofika na kusimama pembeni yake katika eneo la tukio.

Polisi waliitwa katika eneo la michezo na mapumziko,na kuelezwa kuwa kuna watoto wanaocheza na bunduki bandia na hawakuelezwa ikiwa bunduki hizo zilikuwa halisi.

Polisi wanaeleza kuwa walimtaka Tamir Rice mara tatu kunyanyua mikono juu,akakaidi,lakini familia ya kijana huyo inaeleza kuwa kifo cha Tamir kingeweza kuepukwa,lakini polisi walikuwa wepesi kuamua kumpiga risasi, na wazazi hao wamewataka waandamanaji mjini humo kuwa na amani.