Sudan yataka Unamid kufungasha virago

Image caption Kikosi cha Unamid kimekuwa kikijaribu kuchunguza visa vya ukiukaji wa haki za binadamu, kitu kilichoikera serikali ya Sudan

Kikosi Kinachojumuisha askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na wale wa Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur nchini Sudan, UNAMID, kinasema kinafanya juhudi kuweka mambo sawa baada ya serikali kukitaka kufunga ofisi zake za haki za binadamu katika mji mkuu Khartoum.

Uhusiano baina ya maafisa wa Sudan na UNAMID uliingia dosari , baada ya kikosi hicho kujaribu kuchunguza ripoti ya ubakaji wa wanawake wengi unaodaiwa kufanywa na askari wa serikali .

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanawake wakiwakarabisha wanajeshi waliokuwa wameambatana na afisa mkuu wa uchunguzi

Umoja wa Mataifa ulisema mapema mwezi huu kuwa wanajeshi wa Sudan waliwazuia walinda amani kuingia katika kijiji cha Tabit ambako ubakaji wa wanawake 200 na wasichana uliripotiwa kufanyika.

Hata hivyo ushahidi wa madai hayo haukupatikana kamwe.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wanajeshi wa Unamid wakiwalinda wanawake katika kijiji cha Tabit

Maafisa wa Sudan wanasema bado hawajapoke taarifa zozote kuhusiana na ubakaji huo.

Jimbo la Darfur limekuwa likikumbwa na mgogoro wa kisiasa tangu mwaka 2003 wakati ambapo waasi walianza vita.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Maafisa wa uchunguzi hawakupata ushahidi wa ubakaji wa wanawake wa Tabit kama ilivyokuwa imedaiwa

Kikosi cha Unamid, kina jukumu la kusitisha vita na unyanyasaji wa raia na kwa sasa kina wanajeshi 16,000 wanaoshika doria katika maeneo yanayokumbwa na vurugu Magharibi mwa nchi.

Mzozo unaoendelea katika jimbo la Darfur unachochewa na pande zote husika na hata na makundi mengine mengi yanayounga mkono serikali , waasi na wapiganaji.