Israel yatibua njama ya Hamas

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Bendera za kundi la Hamas

Serikali ya Israel inasema kuwa maafisa wake wa usalama, wamegundua kuwa kundi la Hamas katika ukingo wa Magharibi lilikuwa linapanga kufanya mashambulizi kadhaa mjini Jerusalm.

Inaarifiwa wapiganaji hao pia walikuwa wamelenga kushambulia uwanja wa michezo pamoja na mfumo wa reli.

Maafisa wa asalama wamesema kuwa wamewakamata zaidi ya wapiganaji 30 wa Hamas ambao inadaiwa walipokea mafunzo nchini Jordan na Uturuki.

Hamas inasalia chini ya udhubiti wa Gaza , lakini eneo la Ukingo wa Magharibi uko chini ya udhibiti wa chama cha Fatah chake Rais wa Palestina Mahmoud Abbas.

Kukamatwa kwa wapiganaji hao, kunakuja wakati ambapo kuna hali ya suitofahamu kati ya Israel na Palestina, hali ambayo imeshuhudia mashambulizi mabaya zaidi kati ya pande hizo mbili kwa miaka mingi.

Wiki jana wapalestina wawili, walishambulia Sinagogu mjini Jerusalem na kuwaua watu watano.