Mtandao wa Hamas wavunjwa

Haki miliki ya picha
Image caption Wapiganaji wa Hamas

Maafisa Usalama nchini Israel wamevunja mtandao wa Hamas katika Ukingo wa magharibi.

Mtandao huo ulikuwa ukipanga kufanya mfululizo wa mashambulio yaliyokuwa yakilenga mji wa Jerusalem, ukiwemo uwanja wa mpira wa miguu.

Maafisa hao wa usalama wamesema wamewakamata wanamgambo wa Hamas zaidi ya thelathini ambao wamepata mafunzo kutoka katika nchi za Jordan na Uturuki.

Hata hivyo Msemaji wa Hamas amesema ni wazi kwamba Israel imekuwa ikijaribu kupotosha dunia.

Wiki iliyopita Wapalestina wawili walishambulia sinagogi moja mjini Jerusalem na kuua watu watano.