Uchaguzi wa kwanza wa kielektroniki Namibia

Image caption Namibia ni nchi ya wkanza Afrika kupiga uchaguzi kwa njia ya kieletroniki

Wananchi nchini Namibia wanashiriki uchaguzi wa kitaifa ambao unasemekana kuwa wa kwanza wa kielektroniki barani Afrika.

Chama tawala nchini humo (Swapo) kinatarajiwa kushinda uchaguzi huo huku waziri mkuu Hage Geingob akitarajiwa kunyakua ushindi katika kinyang'anyiro cha urais.

Vyama vya upinzani vilikuwa vimepinga mashine hizo kutoka India ambazo zinatumika kwa kupigia kura , vikisema kuwa ukosefu wa kufuatiliza data vyema kunaweza kuchangia wizi wa kura.

Lakini malalamiko yao yalitupiliwa mbali na mahakama kuu mapema wiki hii.

Takriban wapiga kura milioni 1.2 wanapiga kura katika vituo takriban 4,000 kote nchini humo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Harakati za uchaguzi nchini Namibia

Bwana Hage Geingobni anaeonekana kupendwa sana huenda akanyakuwa ushindi wa Urais.

Maafisa wa shughuli ya upigaji kura watahakikisha kadi za upigaji kura ziko sawa. Katika kijisanduku cha kupigia kura, mpiga kura atachagua chama na mgombea anayempenda katika kituo hicho kwenye kijisanduku cha elektroniki.

Maafisa wa uchaguzi wanaamini kuwa matokeo yatapatikana katika muda wa saa 24 baada ya upigaji kura kumalizika.

Kuna vyama vyenye viongozi wake wanaowania uchaguzi huku vyama sita vikiwasilisha wagombea wa urais.

Chama cha Swapo - ambacho kimekuwa kikishinda uchaguzi tangu mwaka 1990 ambapo nchi hio ilijipatia uhuru,kinatarajiwa kushinda kwa mara nyingine katika uchaguzi wa wabunge.

Mgombea wa chama kikuu bwana Geingob tayari amehudumu kwa mihula miwili kama waziri mkuu na anapendwa na wengi sana.