Wanaume 13 washtakiwa kwa udhalilishaji

Haki miliki ya picha
Image caption Genge la Wanaume waliotekeleza vitendo vya udhalilishaji dhidi ya Wasichana

Wanaume kumi na watatu wameshtakiwa kwa kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji kwa Watoto mjini Bristol, ikiwemo vitendo vya ubakaji na kuwalazimisha watoto wa kike kujiingiza kwenye vitendo vya biashara ya ngono.

Mahakama ya mjini Bristol ilimsikiliza binti wa miaka 16 aliyebakwa na Wanaume watano raia wa kisomali.

Halikadhalika mdogo wake mwenye umri wa miaka 14 alibakwa na mmoja wa wanaume hao, Msichana huyo alipofika kumtembelea Dada yake.

Uchunguzi uliofanywa na Polisi ulibaini kuwa genge jingine la wanaume wenye asili ya kisomali liliwadhalilisha kijinsia wasichana wengine wanne.

Wasichana hao walilipwa pauni 30,au kupewa dawa za kulevya, vilevi na zawadi kwa ajili ya kushiriki vitendo vya ngono na wanaume wenye umri mkubwa wa jamii ya kisomali.

Miongoni mwa walioshtakiwa ,Watu sita walihukumiwa kifungo,wengine saba walitiwa hatiani siku ya jumatano.