Kesi dhidi ya Mubarak yatupiliwa mbali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak.Kesi ya mauaji dhidi yake imetupiliwa mbali na mahakama moja nchini humo.

Mahakama moja nchini Misri imetupilia mbali kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak kutokana na mauaji ya mamia ya waandamanaji wakati wa maandamano ya kumng'atua mamlakani.

Aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani wakati wa uongozi wa Mubarak ,Babib al Adly pamoja na maafisa kadhaa pia wameondolewa mashtaka.

Mubarak alihukumiwa miaka miwili iliopita lakini mahakama ya rufaa ikamuondela kifungo cha maisha gerezani.

Mahakama hiyo pia ilimuondolea rais huyo wa zamani mashtaka ya ufisadi.

Bwana Mubarak tayari anahudumia kifungo cha miaka mitatu kutokana na mashtaka ufujaji wa mali ya uma.