Iraq yabaini wanajeshi hewa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wa Iraq

Uchunguzi wa idara ya kupambana na vitendo vya rushwa nchini Iraq umebaini kuwepo kwa wanajeshi hewa 50,000 katika orodha ya malipo ya mishahara.

Askari hao wajulikanao kama askari mizimu yaani Ghost soldiers hawajawahi onekana kazini japo kuwa mishahara yao ilionekana kuendelea kulipwa kwa watu wasiojulikana.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Iraq ofisi yake imechukua hatua kuhusiana na tatizo hilo na tayari malipo ya mishahara hiyo ya skari hewa imekwisha simamishwa.

Vitendo vya rushwa ndani ya jeshi la Iraq vinatajwa kuchangia kurudisha nyuma vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiislam IS Kaskazini na Magharibi mwa taifa hilo.