Mubarak:Raia waandamana Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Raia wa Misri waandamana kufuatia kuondolewa mashtaka kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak

Vikosi vya usalama nchini Misri vimepambana na karibu waandamanaji 2000 karibu na eneo la Tahrir Square mjini Cairo ambapo mtu mmoja aliuawa.

Maandamano hayo yanafanyika kufuatia uamuzi wa mahakama wa kumuondolea mashtaka aliyekuwa rais wa Misri Honi Mubarak kuhusiana na mauaji ya zaidi ya waandamanaji 200 wakati wa maandamano ya mwaka 2011.

Kweye mahojiano na kituo kimoja cha runinga baada ya hukumu hiyo bwana Mubarak alisema kuwa hajafanya lolote baya.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mubarak akiwa kizimbani wakati wa uamuzi wa kesi yake.Maelfu ya raia wamefanya maandamano kufuatia hatua ya mahakama kumuondolea mashtaka rais huyo wa zamani.

Awali alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini hukumu hyo ikabatilishwa .

Hata hivyo bado yuko kuzuizini baada ya kupatikana na makosa ya ufujaji wa pesa za umma.