Majina ya kiarabu yaenziwa Uingereza

Image caption Zamani jina Oliver ndilo lilikuwa linapendwa sana Uingereza lakini mambo yamebadilika

Utafiti nchini Uingereza Umeonyesha kuwa mwaka huu jina Muhammad ndilo limekuwa maarufu sana linalopewa watoto wavulana na kusukuma jina la Oliver hadi katika nafasi ya pili.

Utafiti huo unaonyesha lionyesha kuwa wazazi wengi wamekuwa wakiwapa wanao majina ya kiarabu, huku jina la kike Maryam likipendwa sana.

Ni la kwanza kati ya mjina 100 yanayopendwa na wazazi kuwapa waoto wao wasichana. Jina Nur limesghika nafasi ya pili miongoni mwa watoto wa kike.

Haki miliki ya picha baby centre
Image caption Kwa watoto wasichana, jina Maryam ndilo linapendwa sana

Majina mengine Omar, Ali na Ibrahim ni miongoni mwa mjina 100 yanayopendwa na kupewa watoto wavulana.

Majina yaliyokuwa yakienziwa sana zamani ya kiingezera na yanayohusishwa na familia ya kifalme, yote yameshuka ngazi na wala hayapendwi sana.