Mvutano kuhusu mali ya Mandela waendelea

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bi Winnie Mandela alichana na hayati Mandela mwaka 1996

Serikali ya Afrika Kusini imepinga hatua ya kisheria aliyochukua aliyekuwa mke wa Nelson Mandelakutaka kupewa umiliki wa nyumba ya hayati Mandela katika mvutano unaoednelea kuhusu mali ya Mandela.

Katika ripoti ya korti,Bi Madikizela-Mandela alisema kuwa Rais wa kwanza mweusi wa Africa Kusini aliandikisha mali hiyo katika jina lake kinyume na sheria.

Mali ya Mandela ina thamani ya dola milioni 4.3.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mandela alimuoa Graca Machel mwaka 1998 alipokuwa anasherehekea miaka 80

Bi Mandela alitalakiwa na hayati mzee Mandela mwaka 1996 lakini alienda mahakamani kutaka mahakama kmpa haki ya kumiliki mali hiyo akisema kuambatana na utamaduni ana haki juu ya nyumba hiyo iliyo kijiji Qunu.

Bwana Mandela alifariki takriban mwaka mmoja uliopita bila ya kumtaja mkewe wa zamani kwa wasia wake.

Wawili hao walikuwa wanandoa mashuhuri sana wa kisiasa kwa miaka 38 hadi walipoachana.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Bwana Zuma aliungana na familia ya Mandela wakati wa mazishi ya hayati Mandela

Bwana Mandela alimuoa Bi Graca Machel mwaka wa 1998 alipokuwa akisheherekea miaka 80 tangu kuzaliwa

Kwenye ripoti iliyoko katika mahakama ya Mthatha, Bi Mandela alisema kuwa Bw Mandela alitumia sharia za ardhi vibaya kwa kujipa ardhi ya kibinafsi

Mawakili wake wanamtaka Rais Zuma na wizara ya maendeleo ya vijiji kutoa stakabadhi rasmi zinazoonyesha ardhi hiyo ni ilimilikiwa na Bwana Mandela

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Nyumba ya Mandela inayong'ang'aniwa iko katika kijiji cha Qunu

Bi Madikizela-Mandela anaamini kuwa ardhi hiyo ni yake na alikabidhiwa na mfalme wa Aba Thembu Buyelekhaya Dalindyebo wakati Bwna Mandela alipokuwa gerezani. Anadai kuwa Mandela likwenda kinyume na sheria kujipa umiliki wa ardhi hiyo

Mzee Mandela alitoka jela mwaka 1990, miaka 27 baada ya kufungwa na kuchaguliwa kuwa Rais wa kwanza mafrika nchini humo mwaka 1994.