Kichanga chaokotwa ufukweni Sydney

Haki miliki ya picha k
Image caption Polisi wakiwa katika ufukwe wa Maroubra alikofukiwa Mtoto

Polisi nchini Australia wametoa wito kwa mama wa Mtoto aliyepatikana amefukiwa kwenye mchanga katika ufukwe wa Maroubra mjini Sydney, kujisalimisha kwa Polisi.

Mwili wa mtoto uliogunduliwa na watoto wawili ulikuwa umefukiwa kwa takriban umbali wa sentimeta 30

Polisi wamesema hawakuweza kufahamu mara moja umri na jinsia ya mtoto, kwa kuwa mwili wake ulikua umeoza, mwili huo utafanyiwa uchunguzi.

Tukio hilo limekuja wiki moja baada ya mtoto mchanga kukutwa katika mtaro mjini Sydney.

Mama wa Mtoto huyo anashutumiwa kwa kosa la jaribio la mauaji na Kesi yake itasikilizwa tarehe 12 mwezi huu.