Baraza lote la mawaziri lajiuzulu Taiwan

Image caption Waziri mkuu Jiang Yi-huah alitia saini barua ya kujiuzulu lakini kawasihi mawaziri weke kuendelea na kazi

Baraza lote wa mawaziri 81 mchini Taiwan limejiuzulu kufuatia matokeo mabaya ya chama tawala kwenye uchaguzi.

Chama hicho KMT kilipoteza maeneo tano kati ya sita kwenye kisiwa hicho katika uchaguzi ambao ulionkekana kama kura ya maoni ya sera za rais Ma Ying-jeou dhidi ya China.

Wazi mkuu wa Taiwan naye pia amejuluzulu.

Waandishi wa habari wanasema kuwa wapiga kura nchini Taiwan wanahofu kuwa sera za raii zinawasongesha karibu na China ambayo inadai kuwaTaiwan ni sehemu yake.

Uchaguzi ulionekana na wengi kama wananchi kukataa sera ya chama hicho ya kutafuta ushirikiano zaidi na serikali ya China.

China na Taiwan zimetawaliwa vitafauti tangu mwishoni mwa vita vya wenyewe kwa wenyewe huku China ikiiona kama mkoa ulioasi serikali.

Mwandishi wa BBC Cindy Sui mjini Taipei anasema huku wengi wakizungumzia zaidi uhusiano wa kibiashara na Taiwan wengi wa wananchi wa kawaida hawajanufaika sana na uhusiano huo.

Pia kuna wasiwasi kwamba kisiwa hicho kinategemea sana jirani yake kiuchumi hali ambayo huenda ikaathiri uhuru wa Taiwan.

Mawaziri hao sasa watahudumu katika serikali ya mpito hadi pale waziri mkuu mpya atakapoteuliwa na kisha kuteua baraza jengina la mawaziri.