Pakistan:elimu afya ya uzazi ni ngumu

Image caption Kipindi cha Televisheni huwapa fursa watu kueleza maswala mbalimbali yahusuyo afya

Ngono ni neno linaloonekana kuwa haramu nchini Pakistan, neno hilo huhusishwa na dhambi,mtu huonekana mkosefu na ni tendo la aibu.

Lakini Televisheni ya nchini humo ilivunja miiko hiyo kwa kuonesha kipindi ambacho watazamaji walishiriki kwa kupiga simu kujadili maswala ya Ngono na afya.

Katika nchi ambazo kumekuwa na hofu ya masharti kidini iliyotawala katika maisha ya watu kwa kiasi kikubwa,kunahitaji ujasiri mwingi kuwafanya watu wawe wawazi kuhusu maisha yao ya ngono.

Katika kipindi cha Televisheni mtu mmoja alipiga simu na kuuliza ''Marafiki zangu walio kwenye ndoa wananiambia nguvu za kiume hupungua miezi michache baada ya ndoa je ni kweli?''

Kipindi kiitwacho 'Clinic Online' kinatangazwa na Televisheni ya HTV (Health Tv),Televisheni hii huongelea maisha ya kila siku ya Raia wa Pakistani wakigusia maswala ya afya na mtindo wa maisha.

Kipindi hiki kinathibitika kuwa maarufu kina wachangiaji wengi ambao hupiga simu, wanaume kwa wanawake, nchini Pakistani.

Maswala mengi huibuliwa kuhusu maradhi ya zinaa na utasa pia maswali kuhusu, kujamiiana, ukubwa wa maumbile na kuridhishwa na tendo.

Image caption Dr.Nadeem Siddiqui huuliza maswali ili kubaini tatizo

Dr Nadeem Siddiqui, yeye ni mtangazaji wa kipindi hiki, huuliza maswali kadhaa kwa mwenye shida ili kuweza kubaini tatizo.

Daktari huyu hutoa majibu mazuri ya maana kwa watazamaji lakini wakati mwingine hupata taabu huvuka nje ya mstari na kutoa majibu yasiyo ya kitabibu kwa wapiga simu wanawake kwa mfano husema ''sali sana mara tano kwa siku, jiepushe kuangalia au kusoma vitu visivyo na maadili mazuri mitandaoni, pia soma maandiko ya dini na tatizo litaisha''.

Ushauri wa mashaka.

Hali hii ni tatizo, wakati kipindi aghalab hutoa fursa kwa watu kuongelea kuhusu maswala ya afya, lakini ushauri waupatao wakati mwingine huwa na mashaka.

Dr Javed Usman amesema Madaktari wengi nchini Pakistan hawana utaalamu wa kupambana na matatizo ya afya ya Ngono, kwa kuwa mitaala yao haielezi maswala hayo kabisa, hali inayofanya madaktari kuegemea kutoa ushauri kwa kuegemea kwenye maswala ya kimaadili zaidi, wakiangalia tamaduni, imani za kidini na sio ushauri wa kitabibu.