Cosby ashtakiwa kwa dhuluma za kimapenzi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mwanamitindo mashuhuri pia alidai kuwa Cosby aliwahi kumdhulumu kimapenzi

Mwigizaji na mchekeshaji mkongwe wa Marekani Bill Cosby ameshitakiwa kwa kumdhalilisha mwanamke anayedai kuwa alibakwa na mwigizaji huyo alipokuwa na umri wa miaka 15.

Katika kesi hio bi Judy Huth, anadai kuwa Cosby alimdhulumu kimapenzi katika nyumba moja ya kifahari ambako kulikuwa kunafanyika kipindi cha Playboy mjini Los Angeles mwaka 1974 na kumwambia adanganye kuhusu umri wake.

Wakili wa Cosby, hajaweza kutoa tamko lolote kuhusu kesi hiyo.

Cosby, mwenye umri wa miaka 77, amekua akikabiliwa na madai mapya kila kukicha baadhi ya wanawake wakisema aliwalawesha kabla ya kuwabaka au kuwadhulumu kimapenzi.

Bado hajafikishwa mahakamani kuhusiana na madai yote yaliyowasilishwa dhidi yake ambayo mawakili wake wanadai ni uongo na porojo tupu.

Kesi iliyowasilishwa na Bi Huth inasema kuwa yeye na rafiki yake aliyekuwa na miaka 16 walikutana na Cosby wakati akirekodi filamu flani na baadaye akawaalika kwenda naye katika uwanja wake mdogo wa tenisi, kabla ya kuwapeleka katika nyumba hio ya Playboy Mansion.

Bi Huth anadai kuwa alifanyiwa vitendo vya mapenzi kwa lazima.

Kesi hio, inaonyesha kuwa wasichana hao wawili waliambiwa wadanganye kuhusu umri wao.

Malalamiko ya mwanamke huyo yanasema kuwa alisumbuka sana kimawazo na kwamba anataka kulipwa kwa yote aliyopitia.

Kesi nyingine inayomkabili Cosby ni ya mwanamke mwingine aliyedai pia kudhulumiwa kimapenzi na mwigizaji huyo.

Mnamo mwaka 2005 mwanamke mwingine alidai kuwa Cosby alimlewesha kwa dawa za kulevya na kuanza kumlazimisha kushiriki naye vitendo vya ngono ingawa mwanamke huyo hakumshitaki mahakamani badala yake waliafikia makubaliano nje ya mahakama.

Madai hayo mapya dhidi ya Cosby yametolewa siku moja tu baada ya Cosby kujiuzulu kutoka kwa bodi ya chuo kikuu cha Philadelphia,ambako alikuwa mwanafunzi where he was once a student, amid the allegations.

Baadhi ya vyombo vya habari vilivyokuwa vimepanga kufanya vipindi kadhaa na Cosby vimesitisha mipango hio kwa muda.