Droo ya kombe la Afrika kufanyika leo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Droo ya kombe la mataifa ya Afrika mwaka 2015 kufanyika leo usiku mjini Malabo nchini Equitorial Guinea

Mabingwa wa zamani Zambia na waandalizi wa kombe la bara Afrika Equitorial Guinea ni miongoni mwa timu zitakazoorodheshwa katika droo ya kombe hilo la mwaka 2015 Jumatano usiku.

Shirikisho la soka barani Afrika CAF tayari limezigawanya timu hizo 16 katika makundi vyungu vinne vya kinyang'anyiro hicho cha january 17 hadi februari 8.

Hatua hio ilifanyika kulingana na utendaji wa timu hizo katika awamu tatu ya michuano hiyo na mechi za kufuzu katika kipindi hicho hicho.

Miongoni mwa vitu ambavyo vilitiliwa mkazo ni matokeo ya mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2014.

Droo hiyo ambayo itabuni makundi manne yanayoshirikisha timu moja moja kutoka kila chungu itafanyika mjini malabo jumatano usiku.

Ghana na Ivory Coast ni timu nyengine kubwa huku washindi wa pili wa mwaka 3013 Burkina Faso wameorodheshwa katika kundi la Pili.

2015 Nations Cup :Timu zilivyowekwa.

Pot 1: Equatorial Guinea, Ghana, Ivory Coast, Zambia

Pot 2: Burkina Faso, Mali, Tunisia, Algeria

Pot 3: Cape Verde, South Africa, Cameroon, Gabon

Pot 4: Guinea, Senegal, DR Congo, Congo