Zawadi ya kufuli lililofungwa - Mahakama

Kumekuwa na hali ya kulaumiana baina ya mahakama nchini tanzania na vyombo vya habari ,huku wamiliki wa vyombo vya habari wakiilaumu mahakama kwa ukimya hasa yanapokuja masuala ya kutolewa ufafanuzi.

Hayo yamebainishwa katika mkutano uliojumuisha pande mbili hizo,uliofanyika mjini dar ambapo kwa upande wake mahakama imedai haikutendewa haki .Ni miaka mingi sasa kumekuwa na pengo la taarifa wazi baina ya pande mbili hizo, kiasi cha kufikia baraza la habari tanzania kuwatunuku mahakama tuzo ya kufuli lililofungwa, tuzo ambayo mahakama inalalama kuwa haikutendewa haki wala kupewa nafasi ya kujitetea.

Kwa upande wa vyombo vya habari, huu ni mkutano wa kwanza mkubwa wa aina yake unaotarajiwa kupunguza ufa wa mashauriano na mahusiano ya kikazi kati ya vyombo vya habari na mahakama baina ya mihimili hii miwili kukutana na kukaa pamoja .mkutano ukatiwa uzito jaji mkuu wa mahakama kuu ya tanzania mohamed othman chande alikuwepo ,majaji wa mahakama ya rufaa na maafisa wa ngazi za juu wa makama walihusika pia .Ni haja ya wananchi kuwa na imani na vyombo hivyo , demokrasia ,utawala bora na utoaji haki vyote huzalishwa na wananchi ambao hutaka utawala wa demokrasia na utawala wa.

Hoja mbalimbali na mpya ziliibuka katika mkutano huo na makama ikaahidi kwenda kuzifikiria na kuchukua hatua mjadala mkubwa ni juu ya vyombo vya habari kutaka ruhusa ya mahakama kuingia na vitendea kazi vyao katika baadhi ya kesi jambo ambalo tanzania halijawezekana lakini africa kusini katika kesi maarufu ya mauaji iliyokuwa ikimkabili mwanariadha maarufu oscar pistorius imewezekana, marekani katika kesi ya oj simpson pia iliwezekana pasipo ukinzani haya ni baadhi ya mambo yanayowapa dukuduku waandishi wa tanzania kuataka na wao wawaoneshe jamii kesi zinazo vuta hisia zao.