Ukatili wa kijinsia Jeshini ukomeshwe

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuk Hagel

Waziri wa ulinzi wa Marekana anayeondoka madarakani Chuck Hagel amesema wizara yake imepiga hatua katika kukomesha ukatili wa kijinsia ndani ya jeshi.

Hagel amesisitiza kuwalinda wanaotoa taarifa za kufanyiwa ukatili na wahusika wa vitendo hivyo mara baada ya kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.

Hata hivyo amewasilisha ripoti ya utafiti inayoonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 yawaliowahi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinisia walifanyiwa ukatili mara baada ya kutoa taarifa.

Ripoti ya awali ya vitendo vya ukatili huo kwa mwaka huu ilionyesha kuwa ni asilimia 19 tu ya vitendo hivyo ndani ya jeshi ikiwa imepungua kwa kwa zaidi ya asilimia 25 kwa miaka miwili iliyopita.